TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 01.04.2014.
·
BIBI WA MIAKA 68 AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA
TUHUMA ZA KISHIRIKINA.
·
MZEE WA MIAKA 62 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZIDIWA
NA MAJI YA MTO SAZA.
·
MTOTO WA MIAKA 02 AMEKUTWA AMEKUFA MAJI BAADA YA
KUTUMBUKIA NDANI YA KISIMA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
BIBI WA MIAKA 68
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BELTA
SANZIA MKAZI WA MAWENI AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU KINACHODHANIWA KUWA
SHOKA KICHWANI, MKONO WA KULIA NA KUTOBOLEWA SEHEMU ZA UBAVU WA KUSHOTO NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LA KUSITIKISHA LIMETOKEA MAJIRA YA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 31.03.2014 HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MAWENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA
BAADA YA MAREHEMU KUTUHUMIWA KUWAROGA WANAKIJIJI WENZAKE.
MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI PEKE YAKE KATIKA NYUMBA YAKE.
JUHUDI ZINAENDELEA KUWASAKA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA
MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE
NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MZEE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUCHAGULA MAENZEKA (62) MKAZI WA KITONGOJI CHA KININGA AMEKUTWA AMEKUFA MAJI NDANI YA
MTO SAZA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.03.2014 MAJIRA YA SAA 09:30
ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KININGA, KIJIJI NA KATA YA SAZA, TARAFA
YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA KIFO HICHO NI MAREHEMU
KUSHINDWA KUYAMUDU MAJI YA MTO HUO KUTOKANA NA ULEVI HALI ILIYOPELEKEA KUSOMBWA
NA MAJI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI WANAPOVUKA MITO HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWANI NI HATARI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
TABIA YA KUNYWA POMBE KUPINDUKIA KWANI NI HATARI SI TU KWA AFYA ZAO BALI HATA
KWA MAISHA YAO.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
MTOTO MDOGO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JULIETA CHRISTIAN (02) MKAZI WA SAZA
AMEKUTWA AMEKUFA MAJI NDANI YA KISIMA KILICHOPO JIRANI NA NYUMBA WANAYOISHI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:00
ASUBUHI KATIKA KITONGOJI CHA KATI, KIJIJI NA KATA YA SAZA, TARAFA YA
KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU ALIBAKI PEKE
YAKE NYUMBANI BILA MWANGALIZI YEYOTE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO ILI
KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. AIDHA ANATOAN WITO KWA JAMII KUFUNIKA
VISIMA VILIVYOWAZI, KUFUKIA MADIBWI NA MASHIMO KWANI NI HATARI KWA WATOTO
WADOGO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Signed by:
[AHMED Z.
MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon