Wivu wa Mapenzi Wapelekea Aukate Uume wa Mumewe



NewsImages/6867538.jpg

Catherine Kieu

Mwanamke mmoja wa nchini Marekani anakabiliwa na kifungo cha muda mrefu jela baada ya kuukata uume wa mumewe kwa kisu cha inchi 10 baada ya kugundua kuwa mumewe alikuwa kwenye mahusiano na mpenzi wake wa zamani.

"Maisha yangu yaliisha pale alipoukata uume wangu", alilalama mume wa mwanamke huyo alipokuwa akiiambia mahakama mjini Orange County, California nchini Marekani.

Catherine Kieu mwenye umri wa miaka 50 anakabiliwa na kifungo cha muda mrefu jela baada ya kuukata uume wa mumewe na kumuacha akiwa amefungwa na kamba kitandani akipigania maisha yake huku akivuja damu nyingi sana.

Mahakama iliambiwa kuwa Catherine alimwenyesha mumewe madawa ya kulevya na kisha kumfunga na kamba kitandani kabla ya kutumia kisu kikali cha inchi 10 kuukata kabisa uume wa mumewe na kisha kuutupa.

Mahakama ilisikilizishwa sauti ya mwanamke huyo akishangilia kwa kusema "Unastahili, unastahili". Catherine alitegesha kifaa cha kurekodi sauti chumbani kabla ya kufanya shambulio hilo.

Catherine alichukua uamuzi wa kuzifyeka mali hizo muhimu za mumewe baada ya kugundua kuwa mumewe alikuwa na uhusiano wa siri wa kimapenzi na mpenzi wake wa zamani.

Madaktari walishindwa kuunganisha tena uume wa mumewe na kubakia na uamuzi wa kumtengenezea njia ya kumwezesha aweze kujisaidia haja ndogo bila tabu.

"Aliniua siku ile aliyonikata uume wangu", alisema mume wa Catherine akiiambia mahakama na kuongeza "Sitaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi tena".

"Ninachokumbuka ni kuwa nilishtuka toka kwenye usingizi mzito na kujikuta nikiwa nimefungwa kwa kamba kitandani huku nikiwa kwenye maumivu makali sana", aliongeza mume wa Catherine.

Mwanasheria wa mume huyo aliongeza kuwa mteja wake alikuwa ameishafungua madai ya kutaka kuivunja ndoa yao mahakamani kutokana na mateso na matusi aliyokuwa akifanyiwa na mke huyo. Waliendelea kuishi nyumba moja huku kesi hiyo ya kuvunja ndoa yao ikiendelea mahakamani.

Catherine amekanusha mashtaka aliyofunguliwa akijitetea kuwa ana matatizo ya akili. Hukumu ya kesi hiyo itatolewa ndani ya wiki mbili zijazo

 

Previous
Next Post »