TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 26.03.2014.





Ø  JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LAMSHIKILIA MTU MMOJA   AKIWA  NA BHANGI KILO 1.


Ø  JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LA MSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUPATIKANA NA MALI YA  WIZI [PIKIPIKI]. 


KATIKA MSAKO WA KWANZA:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA LUSAKO KALONGOTI  [30]  MKAZI WA USHIRIKA -TUKUYU BAADA YA  KUKAMATWA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA KILO MOJA [01].

MTU HUYO ALIKAMATWA TAREHE 25.03.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA ENEO LA STENDI YA KIWIRA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. MTUHUMIWA HUYO NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI ALIKAMATWA AKIWA ANASAFIRISHA KWENYE GARI LA ABIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.646 BQD AINA YA  TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKITOKEA KYELA KUELEKEA MBEYA MJINI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WANAOLIMA ZAO HARAMU LA BHANGI AU KUSAFIRISHA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA MSAKO WA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALPHONCE MWAZEMBE  [21]  MKAZI WA KIJIJI CHA ILEMBO - VWAWA WILAYA YA   MBOZI  BAADA YA  KUKAMATWA AKIWA NA PIKIPIKI MOJA T.548 CBN AINA YA  T-BETTER AMBAYO INADAIWA KUWA NI MALI YA  WIZI.
AIDHA ASKARI HAO WALIKAMATA PIKIPIKI NYINGINE T.167 BLK AINA YA SUN-LG AMBAPO MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KUITELEKEZA BAADA YA KUWAONA ASKARI KWANI PIA PIKIPIKI HIYO ILIISHIWA MAFUTA . PIKIPIKI ZOTE MBILI ZIMETAMBULIWA NA WAMILIKI HALISI.

 TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 25.03.2014 MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI KATIKA KIJIJI CHA HANSEKETWA, KATA NA TARAFA YA VWAWA   KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA KUTUMIA NJIA ZA MKATO, KWANI HUWEZI KUPAMBANA NA UMASIKINI WA KIPATO KWA NJIA ZA MKATO BADALA YAKE WANANCHI WAFANYE KAZI HALALI KWA LENGO LA KUPATA KIPATO HALALI IKIWA NI PAMOJA NA KUNUNUA MALI HALALI KATIKA SEHEMU HUSIKA. PIA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI NA KWA WAKATI KUHUSIANA NA UHALIFU NA WAHALIFU.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »