Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine zaidi ya Elfu SITA kukosa makazi kufuatia nyumba zao kuezuliwa na maji huku nyumba 96 zikiwa zimesombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa ARUSHA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya ARUSHA,FIDELIS LUMATO,amesema mpaka sasa jumla ya watu 480 hawana makazi kabisa na sasa wamehifadhiwa katika katika maeneo mbali huku serikali ikiangalia namna yakuwasaidia.
Baadhi ya watu waliakumbwa na mafuriko katika wilaya ya ARUMERU mkoani ARUSHA ambao wanatoka katika vijiji vya TEMI YA SIMBA na BWAWANI wakiwa wamejihifadhi kufuatia nyumba zao kubomolewa na mafuriko huku mashamba yao yakiwa yameharibiwa vibaya pamoja na baadhi ya mifugo yao kufa ambapo tayari serikali kupitia wafadhili mbali mbali wameanza kuwapatia misaada wakazi hao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya ARUSHA,FIDELIS LUMATO akizungumza mara baada yakukabidhi misaada mbali mbali iliyotolewa kwa wananchi hao,ameomba viongozi wa vijiji kuhakikisha kila mwananchi aliyekumbwa na tatizo hilo anapata msaada
EmoticonEmoticon