Hii ni ajali iliyotokea mchana wa March 21 nje ya gheti la kutokea kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo Bus Terminal na imehusisha lori lililofeli breki na kwenda kugonga magari 5,mpaka sasa idadi kamili ya majeruhi na watu waliopoteza maisha haijapatikana.
Jeshi la Polisi tayari wamesha chukua hatua za awali ikiwa ni pamoja na kuwapeleka majeruhi hospitali na kutoa magari yaliyosababisha ajali hiyo,kwa taarifa za awali inasemekana Dereva wa lori hilo alikimbia mara baada ya kutokea ajali hiyo.Ajali hiyo imehusisha magari 6 likiwemo UDA
EmoticonEmoticon