Ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani
Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa
kuhusika na ujambazi uliofanywa dhidi ya Dr. Sengondo Mvungi aliekua mjumbe wa
Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Taarifa inasema Dr Mvungi amefariki dunia akiwa mahututi
hospitalini nchini Afrika Kusini muda mfupi uliopita na taarifa kutumwa
nyumbani Tanzania ambapo wafanyakazi wenzake ofisi ya tume ya mabadiliko ya
katiba wameambiwa wakae karibu na simu zao ili kikitokea chochote kingine
wafahamishwe.
Tayari
viongozi mbalimbali kama Mh. Warioba, Katibu wa tume, naibu na watumishi
wengine wachache wamekwenda nyumbani kwa marehemu.
EmoticonEmoticon