TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19. 10. 2013.






WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA ,KATA YA  KIWIRA TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA  RUNGWE   MKOA WA MBEYA. GOD S/O ADAMU, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA JIJINI MBEYA, ALIUAWA  BAADA YA  KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE NA MAGONGO KISHA MWILI WAKE KUCHOMWA MOTO. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA PIKIPIKI T.827 CKB AINA YA KINGLION ALIYOIIBA NYUMBANI KWA BABA YAKE MDOGO NICODEMUS S/O JACKSON MWALUPASO, SIKU YA  TAREHE 17.10.2013 MAJIRA YA  SAA 08:00HRS NA KUIFICHA PIKIPIKI HIYO KWENYE NYUMBA AMBAYO HAIJAMALIZIKA [PAGALE]. MSAKO MKALI DHIDI YA WAUAJI UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, NA BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.

WILAYA YA  MBOZI – KUPATIKANA NA SILAHA BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 19.10.2013 MAJIRA YA  SAA 01:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGAMBA, KATA YA  ISANSA, TARAFA YA  IGAMBA WILAYA YA  MBOZI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA SELIDA D/O TUSENJE, MIAKA 32, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGAMBA AKIWA NA SILAHA/BUNDUKI MOJA AINA YA  S/GUN BILA KIBALI.MBINU NI KUIFICHA SILAHA HIYO NDANI YA  CHUMBA ANACHOLALA.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KUFUATA UTARATIBU KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU AU KIKINDI KINACHOMILIKI SILAHA BILA KIBALI /TENGENEZA SILAHA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI  WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »