TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06. 09. 2013.





WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO.

HUKO KATIKA KJIJI CHA SELEWA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.535 BPN AINA YA TOYOTA NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA LAMECK S/O MADIHANI, MIAKA 45, MKINGA, MKAZI WA MLOWO LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI T.525 BTN AINA YA  JINGCHENG AITWAE  BARAKA S/O KAMWELA, MIAKA 24, MNDALI, MKAZI WA MLOWO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI MLOWO TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

.
.



Signed by
 [ DIWANI  ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »