TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 25. 09. 2013.





 WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.   
               
MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO KATIKA PORI LA KIJIJI CHA MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. FESTO S/O LUKUMAI, MIAKA 19, MMANG’ATI, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KIBABA ALIKUTWA  AMEUAWA KWA KUCHOMWA MKUKI MGONGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MAREHEMU ALIKWENDA ENEO HILO KUMTAFUTA MKE WAKE ALIYETOROKEA MAENEO HAYO.  CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTU ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA
                                                           MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO NZOVWE BARABARA YA MBEYA /TUNDUMA JIJI NA MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI  NA MWENDESHAJI ASIYEFAHAMIKA,  ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU OBED S/O MWALULUSA,  MIAKA 50, KYUSA ,MKAZI WA NZOVWE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI YAKE MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.

WILAYA YA RUNGWE -WATUHUMIWA AROBAINI WANATARAJIA
                                                                KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO
                                                               NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA     
                                                               FUJO/KUFUNGA BARABARA KUU          
                                                                MBEYA/TUKUYU KWA MAWE NA MAGOGO.
  
                                                                                                                                                                         

MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA KATI YA SAA 18:00HRS HADI SAA 22:00HRS HUKO KATIKA KATA YA KIWIRA VITONGOJI VYA KIBUMBE, MPANDAPANDA, KIWIRA – KATI NA KARASHA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WALIFANYA FUJO KWA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU WAKITUMIA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO ILI MAGARI YASIPITE NA KUSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO. THAMANI HALISI YA UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO KUFAHAMIKA. HATA HIVYO KATIKA TUKIO HILO GARI T.335 CBE AINA YA  TOYOTA L/CRUISER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUKUYU LIKIWA LIMEBEBA MIILI YA  MAREHEMU WATATU LILIGONGA MAWE YALIYOKUWA YAMEWEKWA BARABARANI NA WATU HAO KISHA KULIGONGA GARI T. 771 BBE AINA YA  TOYOTA COASTER NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU WAWILI  NA UHARIBIFU KWA MAGARI YOTE MAWILI. CHANZO  CHA VURUGU HIZO  NI MADAI YA  KUONGEZEWA USHURU WA MAZAO [NDIZI] KUTOKA TSHS 100/= ULIOANZA KUTUMIKA TANGU MWAKA 1989 NA KUFIKIA TSHS 200/= WAKISHINIKIZA URUDISHWE USHURU WA ZAMANI NA  KUFUATIA VURUGU HIZO JUMLA YA  WATUHUMIWA 40 WAMEKAMATWA NA WANATARAJIA KUFIKISHWA MAHAKAMA YA  WILAYA RUNGWE  LEO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUWA CHANGAMOTO KATIKA JAMII HAZIWEZI KUTATULIWA KWA KUWEKA MAGOGO NA MAWE BARABARANI BADALA YAKE WATAFUTE UFUMBUZI KWA KUWASILISHA MATATIZO  KERO NA MAONI  YAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA NA KUKAA  MEZA YA  MAZUNGUMZO ILI KUPATA UFUMBUZI KWA KUZINGATIA HOJA. AIDHA ANASISISTIZA KUWA KUFUNGA BARABARA KUNALETA MADHARA KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA WAKIWEMO WAGONJWA, WASAFIRI, WAGENI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI PIA KUSAFIRISHA MAITI KAMA ILIVYOTOKEA KATIKA GARI T.335 CBE NA KWAMBA JESHI LA POLISI KAMWE HALITASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATU /KIKUNDI CHA WATU WATAKAOSABABISHA UVUNJIFU WA  AMANI.KWA SASA HALI YA ENEO HILO NI SALAMA.


WILAYA YA  MBOZI  - KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA  SAA 05:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGAMBA WILAYA YA  MBOZI  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA AGATHA D/O MSYANI,  MIAKA 18, MNDALI, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE META SEKONDARI, AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA  UZITO WA GRAM 250. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA 
                                                                     MOSHI [GONGO]

MNAMO TAREHE 24.09.2013 MAJIRA YA SAA 21:30HRS HUKO KATIKA KLABU CHA MAKONDEKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA BELIN S/O JAFARI, MIAKA 34, MSAFWA, MKULIMA NA MKAZI WA MAKONDEKO UYOLE AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI LITA 10. MBINU NI KUFICHA POMBE HIYO KATIKA VIDUMU VIWILI VYA LITA 05. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA  POMBE YA  MOSHI  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.




Signed by:
                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.





Previous
Next Post »