.
|
WILAYA YA MBEYA MJINI
- AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA
KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.
KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA
20:00HRS HUKO SOKOMATOLA BARABARA YA SOKOMATOLA/STENDI KUU JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.223 AGQ AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DUNIA S/O FRANSIS, MIAKA 38, MNGONI, MKAZI WA AIR PORT LILIACHA
NJIA KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO
VYA ABIRIA SITA, KATI YAO WANAUME WANNE NA WANAWAKE WAWILI
AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA ANUANI ZAO. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU SABA WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. JUMA
S/O WARIOBA, MIAKA 32, MKAZI WA SAE 2.
MWANDELA S/O MWAMSI, MIAKA 22, MKAZI WA MAJENGO 3. KAMBI S/O ALLY, MIAKA 32, MKAZI WA IRINGA 4. SELEMAN S/O SHELUKINDO, MIAKA 25, MSAMBAA, MKAZI WA ILEJE 5.NURU S/O SHELUKINDO, MIAKA 32,
MSAMBAA, MKAZI WA ILEJE 6. BAHATI D/O
ALLY, MIAKA 14, MKAZI WA SONGEA NA 7.
DUNIA S/O FRANSIS AMBAO WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO KINAENDELEA KUCHUNGUZWA JAPO TAARIFA
ZA AWALI ZINAONYESHA KUWEPO KWA HITILAFU KWENYE BREAK.. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, NA ANAENDELEA KUHOJIWA. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA WANANCHI KUFIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MIILI YA MAREHEMU.
WILAYA YA
RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
|
MNAMO TAREHE
22.09.2013 MAJIRA YA
SAA 19:00HRS HUKO SOGEA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.131 AVN AINA YA TOYOTA
ESCUDO LIKIENDESHWA NA DEREVA PETER S/O MWAIKEMA, MIAKA 20, KYUSA,
MKAZI WA KIWIRA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI MTAFYA
S/O AFYUSISYE MTAFYA , MIAKA 39, KYUSA, MWALIMU WA RUNGWE S/MSINGI,MKAZI WA
TUKUYU ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI AMBAYO
HAIKUFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI WALA AINA YAKE
NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. CHANZO NI MWENDO KASI WA GARI.
DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.
WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI - AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MPANDA
BAISKELI NA KUSABABISHA KIFO.
BAISKELI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA
17:50HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IPENJA
KATA YA MAENDELEO – USOHA WILAYA
YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.
PIKIPIKI T.559 CDC AINA YA T-BETTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI ILIMGONGA MPANDA BAISKELI PIUS S/O MENGO, MIAKA 15,
MSAFWA, MKAZI WA IPENJA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA
NA KUITELEKEZA PIKIPIKI ENEO LA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEHUSIKA
KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE
MARA MOJA.
WILAYA YA
CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA
16:55HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA TAIFA
YA PITI [PITI GAME RESERVE]
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA KWA
KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA WANYAMA PORI WALIMKAMATA EMANUEL S/O HOLMAN, MIAKA 52,MNYAMWEZI,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA
KITIDA AKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA
GOBOLE KATIKA HIFADHI HIYO
BILA KIBALI. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KOSA LA JINAI.
WILAYA YA
CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA
13:20HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITINDI
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MWASHILINDI
S/O LEMSON, MIAKA 48, MNYIHA,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NNE [04] . MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed
by
[DIWANI
ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon