TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 20. 09. 2013.






WILAYA YA  ILEJE  -  AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA KUSABABISHA
                                      KIFO NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 19.09.2013  MAJIRA YA  SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDOLA WILAYA YA  ILEJE  MKOA WA MBEYA. GARI STK 5485 AINA YA TOYOTA HILUX MALI YA  HALMASHAURI YA  WILAYA YA  ILEJE IDARA YA  UJENZI LIKITOKEA KIJIJI CHA ITALE KUELEKEA ITUMBA  LIKIENDESHWA NA  DEREVA VICENT S/O SCOT, MIAKA 35, MUHA, MKAZI WA ITUMBA  LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI  YENYE NAMBA T. 367 BTB AINA YA T-BETTER    AITWAE CHONDE S/O MWASI MIAKA 32, MNDALI,  MKAZI WA ITUMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPELEKWA HOSPITALI KWA MATIBABU PIA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE WAWILI MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA  AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA.  CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 



WILAYA YA MBOZI  - AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA  SAA 17:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SELEWA BARABARA YA  MBEYA/TUNDUMA  WILAYA YA  MBOZI  MKOA WA MBEYA. GARI T. 598 BTK  AINA YA FUSO TIPPER LIKIENDESHWA NA  DEREVA JAPHET S/O MWASHIUYA, MIAKA 21, MNYIHA, MKAZI WA ILEMBA - VWAWA  LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA BAADA YA  GURUDUMU LA MBELE UPANDE WA KUSHOTO KUPASUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA  MATOKEO S/O STEVEN MWASHIUYA MIAKA 27, MNYIHA,MKULIMA   MKAZI WA ISANGU PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE WATANO AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA  SERIKALI WILAYA YA  MBOZI.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO, GARI LIPO ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIOA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA  ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE  MWENYEWE MARA MOJA.


WILAYA YA  MBEYA MJINI  - KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA  SAA 20:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA MAKUNGURU  JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA GREGORY S/O JOHN, MIAKA 20, KYUSA, MKAZI WA MAKUNGURU  AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 2. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.






                                                                                                                                 ……../2.
                                                                     =  2  =



WILAYA YA  CHUNYA  - KUPATIKANA NA BHANGI.


MNAMO TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA  SAA 14:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MTANILA WILAYA YA  CHUNYA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA STAFORD S/O SOMBA MIAKA 26, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA MTANILA   AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 1. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO NDANI YA  NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


Signed by:

                                                      [ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.











































Previous
Next Post »