WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA
GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 18.09.2013 MAJIRA YA SAA 07:30HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIBISI BARABARA
YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.470
BMN AKQ AINA YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA JAMES
S/O GODFREY, MIAKA 37, MNGONI, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NISSA S/O JIMMI, MIAKA 37, KYUSA, MKAZI WA KATUMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
MAKANDANA - TUKUYU. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
|
WILAYA YA
MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 18.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA KUNYWA – MADIBIRA
WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI
POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOYCE
D/O NYOMI, MIAKA 34, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA KUNYWA – MADIBIRA NA WENZAKE WANNE [04] WAKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 10. MBINU NI KUNYWA POMBE HIYO KATIKA KILABU CHA MTUHUMIWA. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon