Ruto alifikishwa ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu
Majaji katika mahakama
ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC wameahirisha kesi ya naibu Rais wa
kenya William Ruto kwa juma moja ili kumpa mda kurejea nyumbani kushughulikia
hali ya kiusalama inayokumba taifa hilo.
Watu wanoaminika kuwa
magaidi wa Al Shabaab wameteka jumba la kifahari lenya maduka la Westgate
jijini Nairobi na kuwazuilia mateka wakenya kadhaa.
Bwana Ruto anakabiliwa
na mashtaka ya uhalifu wa kibinadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa
2007 nchini kenya.
Ruto na Rais Uhuru
Kenyatta, wanakabiliwa na tuhuma za za uhalifu dhidi ya binadamu baada ya
kudaiwa kuhusika na ghasia za kikabila baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008
ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.
Mahakama iliakhirisha
kesi baada ya kikao cha dharura kuitishwa huku upande wa mashtaka ukisema kuwa
hauna pingamizi lolote ikiwa kesi zitaakhirishwa kwa muda mfupi.
Mwakilishi mmoja wa
mashahidi aliangua kilio mahakamani na kutaka mahakama iweze kumruhusu Ruto
kurejea nyumbani kushughulikia swala hilo la dharura.
''Kutokana na hali
ilivyo na maoni tuliyoyasikia , mahakama inamruhusu Ruto kurejea nyumbani kwa
muda wa wiki moja,'' alisema jaji anayesimamia kesi hiyo, Chile Eboe-Osuji.
"Kwa sasa Ruto
ataruhusiwa kusalia Kenya kwa wiki moja, ila ikiwa atatoa ombi lengine,''
alisema jaji Chile.
Kwa mujibu wa wakili
wa Ruto,Karim Khan, alitarajiwa kuondoka Uholanzi saa tatu asubuhi, saa za
Afrika Mashariki
EmoticonEmoticon