BINTI MWENYE UMRI WA MIAKA NANE AFARIKI DUNIA NI BIBI HARUSI ALIYEOZESHWA NA MUME WA MIAKA 40 NCHINI YEMEN.



BIBI harusi wa miaka nane huko Yemen,amefariki dunia kutokana na michubuko ya ndani aliyoipata usiku wa harusi yake, alitoka damu mpaka kufa baada ya uke wake kutanuka kulikosababishwa na kufanya mapenzi na mume wake mwenye miaka 40.

Mtoto aliyejulikana kwa jina la Rawan,alifariki huko Hajjah,Yemen kutokana na ripoti tulizonazo mtoto huyo alifariki jumapili,septemba 8.

Raia wema sehemu hiyo wanataka kukomesha suala hilo la kuoa wasichana wadogo na waliwaita polisi kuwakamata mume wa yule mtoto aliyefariki na familia yake. Lakini bado ndoa za wasichana wadogo za kulazimisha huko Yemen zinabaki kuwa utamaduni unaokubalika na jamii kwenye vijiji vingi.

Raia hao waliwaita polisi kuja kuwakamata huyo mume mkatili na familia ya mtoto na kuwapeleka kortini ambako haki itatendeka na kesi hiyo itawasaidia kukomesha uoaji wa wasichana wadogo kwenye nchi yao.

Bloggers wa Kuwait  wamemuombea 'bibiharusi' na kumlaani 'bwanaharusi' wakisema ni mnyama mkatili anayetakiwa kuadhibiwa vikali.

 Al Bawaba inaripoti kuwa zaidi ya robo ya wasichana wadogo huko Yemen wanaolewa kabla ya umri wa miaka 15.

Inaongeza kuwa nchi hiyo ilipitisha sheria februari 2009 ambayo iliweka umri wa chini kabisa kuolewa ni 17 lakini hiyo ilikataliwa baada ya watengenezaji wa sheria kusema kuwa sio ya kiislamu.

Mwaka 2010 msichana wa miaka 13 aliyelazimishwa kuolewa alifariki siku tano baada ya harusi yake kwasababu alipata mpasuko wa ndani kutokana na kufanya mapenzi ,ilisema organisation ya haki za binadamu ya eneo hilo.

Chanzo cha world vision kilichotolewa machi kinasema watoto wengine wengi wanaolewa kutokana na umaskini na majanga.
Wazazi ambao wanaishi kwa uoga wa majanga ya asili,vita na kuharibika kwa uchumi huwa wanakimbilia ndoa za aina hiyo kuokoa familia zao.

 Kila siku  wasichana 39,000 chini ya umri wa miaka 18 wanaolewa,kilisema chanzo cha World Health Organization.
Previous
Next Post »