AMBWENE YESAYA NDIYE MUWAKILISHI PEKEE CHANNEL O MUSIC AWARDS


ay_5e5be.jpg

AMEINGIA KATIKA KIPENGELE CHA

 MOST GIFTED  EAST AFRICAN VIDEO


MSANII wa kizazi kipya nchini, Ambwene Yessayah 'AY', ameteuliwa pekee nchini kuwania tuzo ya Channel O (Choamva), kwa mwaka huu zitakazofanyika Afrika Kusini.
Mwaka jana AY aliiwakilisha Tanzania na Afrika Mashariki kwa kuchukua tuzo kupitia wimbo wake wa 'I don't want to be alone' akiwa amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi, Kenya, wanaokwenda kwa jina la Sauti Sol.
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, Jina la AY limetajwa katika kipengele cha 'Most Gifted Male' kupitia video ya wimbo wake wa 'Paty Zone' aliyomshirikisha Marco Chali, pamoja na kipengele cha 'Most Gifted Africa East' kupitia video yake hiyohiyo.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake cha 'Bila Kukunja Goti' ambacho ameshirikiana vema na mkali wa muziki huo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA'.
Mwana FA na AY, kwa sasa wako nchini Kenya kutengeneza video ya wimbo huo ambao unafanya vizuri katika soko la muziki, pamoja na kurekodi zingine mbili ambazo wameshirikiana.
Previous
Next Post »