tiGO kuwezesha wateja wake kiuchumi kupitia promosheni ya Miliki Biashara Yako

Moja kati ya Bajaji 60 ambazo zimeanza kushindaniwa leo katika promosheni ya “Miliki Biashara Yako” kutoka Tigo kwa kuongeza salio ya Tsh 1000 tu kwa siku. Mteja wa Tigo anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kushinda. Kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000 na Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji tayari kwa mteja atakayeshinda kuja kuichukua na kuanzisha biashara yake mara moja.

 Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akionyesha ufunguo wa Bajaji kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji wa Fair Deal auto-dealers, Bw. Anil Dewan kama ishara ya uzinduzi ya promosheni mpya ya “Miliki Biashara Yako” ambayo itawawezesha wateja wake kiuchumi kupitia Bajaji 60 zitakazoshindaniwa kwa muda wa miezi miwili, ambapo kila siku mteja atashinda Bajaji moja.

  Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akionyesha alama ya dole ndani ya Bajaji moja kati ya 60 zitakazoshindaniwa kwa kuongeza salio ya Tsh 1000 tu kwa siku. Mteja wa Tigo anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kushinda.

Kutoka kulia Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji, Anil Dewan na Meneja Bidhaa Khalid Saifullah kutoka Fair Deal auto-dealers, wasambazaji wa Bajaj nchini Tanzania.

Meneja Mbunifu wa Ofa za Tigo Suleiman Bushagama (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu promosheni mpya ya “Miliki Biashara Yako.” Pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, Meneja Mauzo Bw. Israel Gadiel  na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji Bw. Anil Dewan wote kutoka Fair Deal auto dealers wasambazaji wa Bajaj nchini Tanzania.   

-

Dar es Salaam, Julai 18, 2013 – Tigo Tanzania leo imezindua promosheni kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” inayolenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku mteja atajishindia Bajaji moja.

Akitangaza promosheni hiyo katika mkutano na wanahabari, Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga alisema, “Tigo inatambua jukumu lake tulionao katika kuboresha maisha ya Watanzania, na kwa sababu hiyo tumeamua kuzindua promosheni ya aina hii kwa ajili ya kugusa zaidi maisha ya watu. Kwa mara nyingine tena tunawapa wateja wetu sababu ya kutabasamu wakiwa na Tigo kwa kuwapatia nafasi ya kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya “Miliki Biashara Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu watapata fursa ya kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira, pamoja na kutoa huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.”

Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Vile vile mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na hayo, ili kuwapatia urahisi zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa kuongeza salio pitia namna zote zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au kwa vocha ya kawaida.

“Tunaamini kwamba promosheni hii itawapatia wateja wetu sababu nyingine yakutabasamu. Wateja 60 watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji mpya kabisa ambapo wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe. Biashara ya Bajaji ni biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa Bajaji anaweza kuingiza kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000 kwa siku, sawa na Tsh 900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa mwaka,” alielezea Mpinga.

Bw. Mpinga alisema kwamba kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja kuchukua Bajaji yake na kuanzisha biashara yake mara moja,” alimalizia Mpinga.

Previous
Next Post »