“PRESS
RELEASE” TAREHE 19. 07.2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI- KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI
MANAMO TAREHE 18/09/2013 MAJIRA
YA SAA 08:00HRS HUKO KALOBE JIJINI MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA MISAKO
WALIMKAMATA NDUNGUTSE S/O RUTOGE, MIAKA 15, MMALAWI AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA
KIBALI. MTUHUMIWA YUPO MAHABUSU TARATIBU
ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA NYINGINE ZINAFANYIKA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII PINDI WAWAONAPO AU KUWATILIA
MASHAKA WATU WASIOWAFAHAMU KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.
WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 18/07/2013 MAJIRA YA
SAA 14:00HRS HUKO KALOBE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MISAKO WALIWAKAMATA [1] MBWIGA
S/O ESTON, MIAKA 28, MSAFWA, MKULIMA MKAZI WA NZOVWE [2] RASHIDI S/O KAUNDA, MIAKA 26, MNYIHA MKAZI WA KALOBE [3] FRANK S/O DANIEL, MIAKA 17, MSAFWA,
MKULIMA MKAZI WA KALOBE NA [4] PHILIPO S/O KANDEO, MIAKA 29,
MNGONI MKAZI WA NZOVWE WAKIWA NA BHANGI KILO MOJA NA NUSU [11/2] PAMOJA NA MISOKOTO 362 NDANI YA MFUKO MWEUSI WA RAMBO. WATUHUMIWA NI WAUZAJI
NA WATUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon