TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI



“PRESS RELEASE” TAREHE 12. 07. 2013.

WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA MOTO

MNAMO TAREHE 11.07.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO ENEO LA FOREST MPYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. HARRISON S/O RASHID,MIAKA 45,MLAMBYA,MKULIMA MKAZI WA FOREST MPYA ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO KWA NYUMBA YAKE NA KUTEKETEA  YOTE PAMOJA NA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI HUMO . NYUMBA HIYO YENYE VYUMBA VITANO ALIYOKUWA AKIISHI MHANGA NA FAMILIA YAKE IMEJENGWA KWA KUTUMIA MATOFARI NA KUEZEKWA BATI . THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA PIA CHANZO CHA MOTO HUO KINACHUNGUZWA. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOARIFIWA KUTOKEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA TAHADHARI JUU YA MAJANGA YA MOTO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA

WILAYA YA MBEYA – UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU

MNAMO TAREHE 11.07.2013 MAJIRA YA SAA 12:30HRS HUKO ENEO LA META JIJI NA MKAO WA MBEYA. TUMPE D/O MLOPE, MIAKA 45, KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MBALIZI ALINYANG’ANYWA PESA TASLIMU TSHS 15,000,000/= NA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SEBASTIAN S/O SANGA AKIWA NA WENZAKE WANNE WASIOFAHAMIKA. MBINU NI BAADA YA MTUHUMIWA  KUMPIGIA SIMU MHANGA KUWA KUNA MAHARAGE YANAUZWA  ENEO LA MAGEREZA NA MHANGA ALIFIKA ENEO HILO NA KIASI HICHO CHA FEDHA KWA KUWA ANAMFAHAMU MTUHUMIWA NDIPO MTUHUMIWA NA WENZAKE WAKITUMIA GARI NDOGO WALIMUINGIZA MHANGA NDANI YA  GARI HIYO KWA NGUVU KISHA KUMYANG’ANYA  MKOBA MDOGO ULIOKUWA NA PESA NA KUTOWEKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUWA NA TAMAA YA KUJIPATIA MALI/KIPATO CHA HARAKA KWA NJIA ZISIZO HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIKOKIMBILIA WATUHUMIWA HAO AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

 MNAMO TAREHE 11.07.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO ENEO LA MABATINI JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MARIA D/O ELIAS,  MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA MABATINI  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1.5  .  MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA SAMBAMBA NA KUWA HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed By,
[BARAKAEL MASAKI   - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Previous
Next Post »