Taarifa
iliyotolewa na shirika la habari la Uingereza BBC, Julai 8 kuhusu
utafiti uliofanyika nchini Uingereza uliowahusisha watoto 11,000
wakifuatiliwa kuhusu ratiba zao za kulala na kupima uwezo wa bongo zao.
Watafiti
hao walisema ya kwamba wale watoto waliolala baada ya saa tatu usiku na
waliokuwa hawana ratiba maalumu walikuwa na alama za chini kwenye
hisabati na uwezo wa kusoma.
Na
vilevile waliripoti kuwa ni vigumu ubongo kujifunza vitu vipya kutokana
na ukosefu wa usingizi. Walichukua watoto wa kati ya miaka 3, 5 na 7
wakifuatilia uwezo wao wa kujifunza ukilinganisha na ratiba zao za
kulala. Ratiba ilikuwa mbaya zaidi kwa watoto wa miaka 3. Na mpaka
wanapofika miaka saba huwa na ratiba inayoeleweka kati ya saa moja na
nusu usiku na saa mbili na nusu usiku.
Waliokuwa
na ratiba nzuri ya kueleweka walifanya vizuri zaidi katika hisabati na
kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma ukilinganisha na wenzao wasio na ratiba
ya kueleweka na waliokuwa wanachelewa kulala .
Kuhusu
kupungua uwezo wa ubongo athari zilionekana zaidi kwa wasichana
ukilinganisha na wavulana. Utafiti huu uliofanywa na Prof. Amanda Sacker
wa chuo kikuu cha London alisema kuwa vilevile mazingira mabaya ya
familia zetu huweza kupelekea hali hii na aliijumuisha katika sababu za
kupunguza uwezo wa ubongo.
Kitu
Muhimu cha kuzingatia ni watoto kulala mapema na kumbuka bado
hujachelewa, ni vizuri kumuwekea ratiba nzuri ya kulala mtoto, na
hakukuwa na ushahidi wa matokeo kuwa mazuri mtoto akilala kabla ya saa moja na nusu.
Kwa ujumla ili mtoto afanye vizuri darasani ni vema apate usingizi mnono usiku
EmoticonEmoticon