Hatma ya Taifa Stars kucheza fainali za CHAN kujulikana Julai 27 itakaporudiana na Uganda.

STARS

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu, kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Previous
Next Post »