Ikiwa ni wiki moja sasa toka Basi la SUMRY la Mpanda kupata ajali mbaya
na kusababisha Vifo vya watu 9 na kujeruhi wengine zaidi ya 20 na ikiwa
ni siku takribani 4 ndani ya wiki moja Basi jingine la SUMRY linalofanya
safari zake Kati ya Mbeya - Sumbawanga kupata ajali ,mzimu wa ajali
waendelee kuyakumba mabasi ya SUMRY baada ya Leo tena kutokea ajali ya
tatu ikiwa ni wiki moja pekee.
Ajali hiyo imetokea mchana wa Leo mida ya Saa 8 mchana Katika eneo la
Mbuga Yeupe Katika barabara kuu ya Mpanda- Sumbawanga huku ikidaiwa kuwa
dereva aliyesababisha ajali hiyo ni Yule aliyesababisha ajali juzi
Katika basi la SUMRY linalofanya safari zake Kati ya Mbeya - Sumbawanga .
Katika ajali ya Leo inadaiwa hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha.
KWA TAARIFA ZAIDI ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO WETU. Source: www.matukiodaima.com
EmoticonEmoticon