Abiria takriba 40 wanusurika kifo baada ya basi la Mohammed Trans kupata ajali baada ya kumwepa mwendesha pikipiki.


AJALI

Abiria zaidi ya 40 waliokuwa wakitoka Dodoma mjini kuelekea jijini Mwanza leo wamenusurika kufa baada ya basi la kampuni ya Mohammed Trans lenye namba za usajili T 210 APG, kupata ajali kwenye mzunguko (round about) ya peoples klabu mjini Singida.

Baadhi ya abiria wamepata majeraha madogo madogo.

Imedaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki. AJALI 2

 

Previous
Next Post »