Wakati Kim Kardashian na mpenzi wake Kanye West wanategemea kupata mtoto wa kwanza hivi karibuni, couple hiyo hivi sasa inaandamwa na uvumi uliosambaa mtandaoni kuwa Kanye West ni shoga.
Swali linakuja kwamba pamoja na hayo yanayozungumzwa iwe ni ya kweli au ni uzushi lakini Kim K ambaye amebeba kiumbe cha Kanye anajisikiaje na analichukuliaje swala hilo?
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Radar online kuwa Kim hajaamini maneno yanayozungumzwa mtaani kuwa mpenzi wake ni shoga na anachukulia uvumi huo kuwa ni wa kushangaza.
Chanzo kimeendelea kusema uvumi huo unamkasirisha sana mama kijacho sababu unawaletea usumbufu mkubwa kutoka kwa waandishi wa habari, na pia mtu yeyote anapomzungumzia vibaya Kanye inamkosesha sana raha na kumwongezea hasira.
Hivi karibuni Kanye west amezushiwa kuwa na mahusiano na mwanaume aitwaye Riccardo Tisci ambaye wamekuwa wakionekana pamoja mara kadhaa.
EmoticonEmoticon