Ubalozi wa Italia nchini Tanzania wakusudia kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia upasuaji katika hospitali ya St. Gaspar ya Itigi mkoani Singida.

 

Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Perluigi Velardi (wa nne kushoto) akizungumza na vyombo kuhusu onyesho la hiari litakalofanyika leo katika Hoteli ya Golden Tulip kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuisaidia hospitali ya Gaspar ambapo amesema wanategemea watu wengi watajitokeza kununua tiketi ambapo pia watapata fursa ya kufurahia muziki wa Kiitalia kwa burudan itakayotolewa na kundi la “Two Hot Daltonics” kutoka Italia. 

Mwakilishi wa Hospitali ya Rufaa ya St. Gaspar ya Itigo mkoani Singida Gabriele Maneo ( wa pili kulia) akizungumza katika mkutano huo ambapo amesema kwa sasa hospitali hiyo ina uhitaji wa haraka wa kitanda kipya cha kufanyia upasuaji kwa kuwa kilichokuwepo kimeharibika. Ameongeza kuwa kitanda kipya kitakacho gharimu dola 15,000 kitasaidia kuhudumia wagonjwa takriban 600 kwa mwaka ambao wanafanyiwa upasuaji mkubwa na 900 wanaofanyiwa upasuaji mdogo hospitalini hapo.

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Ndege la Egyptair Hany Osman (kulia) akizungumzia hatua ya shirika hilo kuwa mmoja wa wadhamini wa onyesho hilo litakalofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip leo na kuwa madhumuni ni kufanikisha kuchangishwa kwa fedha hizo ili kuwezesha wakazi wa Singida kupata huduma ya upasuaji kwa viwango bora.

Sales & Marketing Coordinator wa Golden Tulip Hotel Catherine Lumbanga akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka watu kujitokeza kwa wingi katika hafla hiyo ambayo itakafanyika kwenye ukumbi wa Marquee wenye hewa safi na utulivu.

Ubalozi wa Italia nchini Tanzania umeandaa onyesho la hiari kwa lengo la kuchangisha dola 15,000 zitakazokabidhiwa kwa Hospitali ya Rufaa ya St. Gaspar iliyopo Itigi mkoani Singida.

Akizungumzia onyesho hilo Balozi wa Italia hapa nchini Bw. Perluigi Velardi amesema lengo la kukabidhi fedha hizo kwa hospitali hiyo ni kuiwezesha kununua kitanda kikubwa cha kisasa cha kufanyia upasuaji mkubwa na mdogo.

Onyesho hilo litafanyika katika hoteli ya Golden Tulip hapo leo tarehe 7 mwezi huu kwa kiingilio cha shilingi 70,000/= ambapo tiketi zinapatikana katika uboalozi wa Itali na Hoteli ya Golden Tulip.

Previous
Next Post »