TAARIFA KWAVYOMBO VYA HABARI LEO KATIKA UKUMBI WA HABARI MAELEZO, TAR 30 MAY 2013.



Shirikisho la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation) kwa kushirikiana na Kamati ya Kuratibu Mazishi ya marehemu ALBERT MANGWEA aliyefariki Afrika ya Kusini akiwa kwenye shughuli zake za kimuziki .

Tunapenda kuwajulisha watanzania kuwa kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa basi mwili utawasili siku ya jumamosi jioni tarehe 1.06.2013.

Baada ya hapo mwili utahifadhiwa tayari kwa maandalizi ya kumuaga siku ya Jumapili saa mbili asubuhi katika viwanja vya Posta/Leaders/Biafra, kimoja kati ya hicho

Siku ya Jumapili jioni safari ya kuusafirisha mwili wa marehemu Morogoro Kihonda kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 03.06.2013.

Tunatambua ambavyo watanzania wanaukumbuka mchango wa marehemu jinsi alivyowahudumia kwa kuwaburudisha hivyo Shirikisho la Muziki   Tanzanuia Kamati ya kuratibu shughuli ya mazishi tunawaomba watanzxania wote kujitokeza kwa wingi siku hiyo katika kumuaga kijana wetu amabaye alikuwa nyota kwetu sote. Namba ya Mchango ni 0754967738 namba ya Keneth Mangwea ambaye ni Kaka Marehemu.


Kwa kuwa kuna gharama kubwa kama vile kusafirisha mwili kutoka Afrika ya kusini na kusafirisha mpaka Morogoro, usafiri, vyakula, viti, matangazo na malazi Tunawaomba watanzania watuchangie kufanikisha msiba huo maana tuna amini kuwa wingi wetu watanzania ndiyo nguvu yetu.

Tunaomba tushirikiane sote kwa PAMOJA katika katika kipindi hiki kigumu. Taarifa zaidi tutawapatia baadae kadri itakavyo bidi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe.

Vile vile tunampa pole mwanamuziki Mgaza Pembe (M TO THE P) na kuomba maombi ya watanzania kumuombea mwanamuziki huyo  ambaye aliyekuwa Afrika Kusini na Marehemu. M TO THE P Mpaka sasa amelazwa huko Afrika Kusini. Tunamuombea apone haraka. Na tunatoa wito kwa watanzania pia kumchangia kwa hali na mali.

Imeandaliwa na ADAM JUMA 0754074323 NA 0658074324 – MSEMAJI WA KAMATI YA KURATIBU MAZISHI NA

Addo November Mwasongwe
Rais1` Shirikisho la Muziki Tanzania
0713396367/0754396367
30th May 2013.
Previous
Next Post »