Diwani
wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka alisema baada ya kupewa taarifa hizo aliamua
kufuatilia na kumbana Mtendaji huyo kuhusu madai hayo ya Wananchi ambapo Mei
23, Mwaka huu alikiri kuhusika na kudai kuwa alipewa Laki saba pekee ambazo
alizikabidhi katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji.
KATIKA
Hali isiyo kuwa ya kawaida Wakazi wa Kitongoji cha Isanzo Mtaa wa Chapwa uliopo
katika Kata na Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Momba Mkoani Mbeya wamefanikiwa
kuzikomboa fedha zilizokuwa zimeliwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo zaidi ya
Shilingi Milion 14.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni katika Mkutano wa hadhara uliofanyika
Chapwa katika Mji huo baada ya baadhi ya wananchi kumtuhumu Mtendaji huyo
kujipatia fedha kinyume na utaratibu kutokana na malipo ya fidia ya eneo la
Kitongoji cha Isanzo lililochukuliwa na Mamlaka ya mapato (TRA) kwa ajili ya
ujenzi wa Nyumba za watumishi.
Kwa
mujibu wa Wananchi waliofika katika mkutano huo uliokuwa ukiongozwa na Diwani wa
kata ya Tunduma Frank Mwakajoka(CHADEMA) walisema chanzo cha Mtendaji huyo
Daniel Sinkonde kula fedha hizo ni kutokana na kufoji majina ya wakazi wa
Kitongoji hicho waliokuwa wakistahili kulipwa fidia kutoka
TRA.
Walisema
wakati Mamlaka ya Mapato ilipohitaji majina ya wakazi hao kwa ajili ya kulipwa
fidia, Mtendaji huyo aliamua kutunga majina sita ambayo aliyapeleka TRA ambapo
Mamlaka hiyo iliandika hundi kwa wahusika ambao baada ya kukabidhiwa fedha zao
walizipeleka kwa Mtendaji ambaye aliwalipa Shilingi Laki 5 kila mmoja kama
kifuta jasho.
Waliongeza
kuwa baada ya kukamilisha kwa zoezi hilo mtu mmoja kati ya Sita ambaye
alijulikana kwa jina la Vasta Choka alilipwa Shilingi laki Tatu badala ya Laki
Tano kama wenzie walivyolipwa ambapo alipojaribu kufuatilia alibaini kudhulumiwa
ndipo suala hilo lilipotinga kwa wananchi na hatimaye kumfikia
Diwani.
Waliyataja
majina yaliyoghushiwa na viwango vya fedha kwenye mabano vilivyolipwa na
Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa ni Elisa Sinkonde (mil 3,281,680/=),John Siwakwi (
Mil 2,387,800/=), Frank Mshani ( Mil 2,740,080/=), Vasta Choka 2,542,680/=),
Jumatatu Silagwe (Mil 1,279,320/=) na Ezekia Kuyokwa (Mil 1,961,400/=) na jumla
yake ni Shilingi Milion 14,192,960/=.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka alisema baada ya kupewa
taarifa hizo aliamua kufuatilia na kumbana Mtendaji huyo kuhusu madai hayo ya
Wananchi ambapo Mei 23, Mwaka huu alikiri kuhusika na kudai kuwa alipewa Laki
saba pekee ambazo alizikabidhi katika Ofisi ya Serikali ya
Kijiji.
Alisema
kutokana na kukiri huko pamoja na kurudisha fedha hizo alienda katika Ofisi za
Mamlaka ya Mapato na kubaini kuwa Mtendaji huyo alikuwa ameshalipwa zaidi ya
Milion 14 kutokana na malipo ya Fidia ya viwanja kwa majina feki
yaliyopelekwa.
Mwakajoka
aliongeza kuwa awali Mtendaji huyo aliahidi kuzilipa fedha zote na kwamba endapo
angeshindwa aliweka nyumba yake kama dhamana nyumba yenye hati ya kiwanja namba
KAL 521 yenye thamani ya Shilingi Milion 30.
Kutokana
na kusuasua huku baadhi ya wananchi kutojua mustakabali wa Mtendaji huyo
waliamua kuitisha mkutano wa Hadhara kwa lengo la kumshinikiza Mtendaji huyo
kuzirejesha fedha zilizobaki ambapo alipofika Mkutanoni alikutwa na Shilingi
Milion 4 tu hivyo wananchi kupandwa na hasira ya kutaka kuuza nyumba
yake.
Baada
ya kutokea kwa mtafaruku huo ndipo alipojitokeza Mfanyabiashara mmoja
aliyefahamika kwa jina la Adolf Mwanyangala kumdhamini kwa kumkopesha Milion 3
na Laki tano ambazo alilipa na kufanikisha kumaliza deni
lote.
Aidha
alipotakiwa kuzungumza lolote Mtendaji huyo aliomba msamaha na kuongeza kuwa
halikuwa kusudio lake na alifanya hivyo kwa bahati mbaya tu na kuwaomba wananchi
wamsamehe.
Pia
wananchi walimwomba Mkurugenzi Mtendaji wa Mji mdogo wa Tunduma kumfukuza kazi
kabisa Mtumishi huyo kutokana na kutokuwa na sifa za utmishi wa
umma.
Picha
na Ezekiel Kamanga Mbeya
yetu
|
EmoticonEmoticon