Mbunge mchungaji Peter Msigwa |
Polisi waliotoka kumkamata mbunge Msigwa leo |
Gari ya mbunge Msigwa kabla ya kukamatwa leo kwa kuhusishwa na vurugu ..........................................................................................
Na Francis Godwin, Iringa
MASAA zaidi ya 6 ya mapambano kupiga mabomu ya machozi na kurushiana mawe kati ya wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga ) na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Iringa yaishia pabaya kwa jeshi la polisi kumkamata mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) na watu wengine zaidi ya 60
Polisi watumia mabom ya machozi kutawanya machinga wapiga mabomu hadi stendi kuu ya mabasi abiria walazimika kutimua mbinu na kuacha mizigo yao katika magari huku machinga hao wakitumia mawe na kuchoma mataili moto barabarani kuvunja vioo vya gari la Zimamoto na kuharibu mali mbali mbali kama njia ya kupambana na polisi
Tukio hilo la Mapambano kati ya machinga na polisi lilitokea leo kuanzia muda wa saa 3 asubuhi na kuendelea hadi saa 8 mchana katika eneo la Mashine tatu mjini Iringa na maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa .
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ambao ulikuwepo eneo la tukio toka saa 12 za asubuhi ya jana alishuhudia kundi kubwa la askari wa FFU wakiwa na gari la maji ya kuwasha ambao wakesha wakilinda eneo hilo .
Askari huo walilazimika kukesha wakilinda eneo hilo kufuatia kauli ya mbunge Msigwa aliyoendelea kuitoa katika mikutano yake ya hadhara mjini hapa kuwhamasisha machinga hao ambao Halmashauri ya Manispa ya Iringa iliwahamisha eneo hilo la mashine tatu na kuwapeleka eneo la Mlandege kabla ya mbunge Msigwa kuwahamasisha kurejea tena eneo hilo.
Kabla ya mbunge Msigwa kufika eneo hilo majira ya saa 3 asubuhi machinga hao ambao walikuwa wamejikusanya makundi madogo madogo bila kupanga biadhaa zao walisikika wakidai kumsubiri mbunge Msigwa kama alivyopata kuwaahidi kuwa atafika eneo hilo kuungana nao kwa kuwa machinga mpya .
Hata hivyo baada ya mbunge huyo kufika akiwa na gari lake la kibunge ambalo lilikuwa lilikokota tela la kuhifadhia mizigo alisimama eneo hilo na kuendeleza msimamo wake wa kuwataka machinga kupambana na baada ya muda alitoweka eneo hilo kabla ya polisi kuanza kuwatawanya machinga hao kwa mabomu ya machozi .
Wakizungumzia hali hiyo ambayo ni ya kwanza kutokea katika mji wa Iringa wakazi wa mji wa Iringa walisema kuwa mbunge na viongozi wengine wa serikali wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kutumia njia nzuri ya kukutana kwa ajili ya kumaliza mvutano huo ambao unaendeshwa kisiasa zaidi.
Festo Sanga alisema kuwa hali ilipofikia ni mbaya zaidi na hivyo busara zinahitajika kwa ajili ya kutatua tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kutazama eneo zuri kwa ajili ya machinga bila kuendelea kuonyeshana ubabe .
Sanga alisema kuwa machafuko yaliyojitokeza leo ni machafuko ambayo wakazi wa mji wa Iringa walikuwa wakishuhudia katika vyombo vya habari katika mikoa mingine ukiacha lile la Septemba 2 mwaka jana lililotokea kijiji cha Nyololo kati ya wafuasi wa Chadema na polisi na kupelekea kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.
“Kweli katika hili mbunge wetu hapaswi kuendelea kulazimisha machinga kuvunja sheria ila anayo nafasi ya kukutana na viongozi wenzake ili kutafuta suluhu ya jambo hilo vinginevyo wanaoteseka na machinga na wale waliokamatwa kwa vurugu hizo ujue wengi waliopigwa mabomu ya machozi si machinga wengine walikuwa wasafiri na badhi yao walikuwa wakielekea makanisani ”
KUhusu kukamatwa kwa mbunge huyo na kuhojiwa na polisi juu ya vurugu hizo Sanga alisema kwa upande wake analipongeza jeshi la polisi kwa kutumia busara zaidi ya kumkamata mbunge kama mhusika mkuu na kuliomba jeshi la polisi kuwaachia wananchi waliokamatwa kwa vurugu hizo.
Huku Sarah Kalinga alidai kuwa chanazo cha machafuko hayo ni mvutano kati ya CCM na Chadema na kuwa ilipaswa vyama vyote viwili kukutana na kuwasaidia machinga badala ya kuwanyanyasa kwa kutumia nguvu kuwabana .
Hata hivyo alisema wao kama walalahoi wanampongeza mbunge wao kwa kuonyesha kuwapigania japo haungi mkono njia inayotumiwa na mbunge ya kuwahamasisha kuvunja sheria na kuwa matatizo na majeraha wanapata wao wananchi na sio mbunge.
Awali mbunge mchungaji Msigwa kabla ya kukamatawa na jeshi la polisi alitoweka katika mazingira tata katika eneo hilo la mashine tatu na kuibukia eneo la chuo kikuu cha Tumaini Iringa ambako kulikuwa na harambee ya kuchangia Kanisa na mgeni rasmi akiwa waziri mkuu mstafu Frederick Sumaye na mara baada ya shughuli hiyo kumalizika ndipo alipokamatwa na polisi na kufikishwa kituo cha polisi.
Kabla ya kukamatwa kwake mbunge Msigwa alizungumza na mwandishi wa habari hizi na kuwa yupo tayari kukamatwa wakati wowote na kuwa kamwe ataendelea na msimamo wake wa kuwataka Machinga kufanya biashara eneo hilo.
Mbali ya kukamatwa kwa mbunge Msigwa kwa kuhusishwa na vurugu hizo pia jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wengine zaidi ya 60 akiwemo aliyekuwa kampeni meneja wa Chadema jimbo la Iringa mjini na mgombea udiwani kata ya kwa Kilosa Abuu Changawa Majeck.
Huku idadi ya majeruhi waliojeruhiwa kwa kupigwa mawe na machinga na badhi ya machinga waliokamatwa kwa vurugu hizo pia wakijeruhiwa vibaya wakati wakipambana na polisi hao.
Taarifa kutoka jeshi la polisi zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda zinadai kuwa watu zaidi ya 60 ndio wamekamatwa hadi sasa na jitihada za kuwasaka wengine waliohusika katika vurugu hizo ambazo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za wananchi unaendelea.
Huku akidai mali mbali mbali zimeharibiwa likiwemo gari hilo la zimamoto mjini Iringa pamoja na uharibifu mwingine mdogo mdogo wa mali za wananchi .
Jeshi hilo la polisi limesema kamwe halipo tayari kumwachia mbunge Msigwa kwa leo hadi hapo atakapofikishwa mahakamani Kesho
MWISHO
|
EmoticonEmoticon