MAKAMANDA
wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya
uhalifu ikiwa na kuweka mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika
kukiuka sheria na taratibu za kazi.
Mkutano
huo unafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya,
lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya usalama na uhalifu wa maeneo katika Mikoa
ya Morogoro, Iringa, Ruvuma, Njombe na Mbeya .
Akizungumzia
mikakati hiyo, Mwenyekiti wa Mkutano Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro,
Ndugu Faustine Shilogile alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni
kujadili matukio ya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali
pamoja na kujadili nidhamu kwa watendaji wa jeshi hilo.
Amesema
Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu
moja hivyo mkutano huu utasaidia kwa wajumbe kubadilishana na kupeana uzoefu wa
kazi,’alisema
Aidha,
amefafanua kuwa jeshi la polisi hivi sasa kupitia baadhi ya askari limekuwa
likikumbwa na matukio ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali
za uhalifu.
Kwa
upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni
mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao hicho kinatarajia kutoka na mikakati
itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu pamoja na ajali
barabarani.
Amesema
mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia njia nyingi kufanya uhalifu na
kukimbilia mikoa ya jirani hivyo mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda
pamoja na wakuu wa upelezi utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao
uliopo
Mkutano
huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza kufanyika Mkoani Iringa na wapili
ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio
mapya.
Na Mbeya yetu
|
EmoticonEmoticon