JANUARY MAKAMBA NAYE AWAPONDA CLOUDS FM KWA KUGOMA KUPIGA "BONGO FLEVA



Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.

Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.

Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
Anonymous
AUTHOR
7 May 2013 at 07:40 delete

Kituo ni chake mimi nadhani alifanya hivyo kwa kile alichoamua kufanya na si kumfurahisha au kumkuna mtu. Kile ni kituo binafsi acheni kumsakama Ruge wa watu

Reply
avatar