Picha .Askofu wa kituo cha maombezi na uponaji cha
Overcomers Power Center (OPC) Dkt Boaz Sollo (kushoto) akimakabidhi tuzo ya
heshima mfano wa ramani ya Tanzania waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
katika hafla ya kuchangia ujenzi wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio
Overcomers Fm ,katika harambee hiyo Lowassa aliahidi kuachangia milioni 15 na
kufanikisha kupata Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo fedha taslimu na ahadi

Na Francis
Godwin
WAZIRI mkuu mstaafu
Edward Lowassa amesema kuwa mbali ya kuwa yeye si tajiri ila bado ataendelea
kufanya kazi yake kwa ukaribu zaidi na jamii ikiwa ni pamoja na kushirikiana na
marafiki zake kusaidia na kuwataka wale wote wenye kusema dhidi yake kuendelea
kusema ila hatarudi nyuma katika kutoa misaada kama njia ya kutafuta baraka za
Mungu.
Lowassa ambae pia
alikabidhiwa tuzo ya heshima kwa ajili ya kuendeleza kulipigania Taifa la
Tanzania ,huku mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh milioni 15 na mbunge wa jimbo
la Ludewa Deo Filikunjombe akichangia milioni 9 kati ya fedha zote zaidi ya Tsh
milioni 75 zilizochangwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kanisa la OPC mkoani
Iringa kama njia ya kuhamasisha amani katika Taifa ametaka watanzania kuwapuuza
wale wote wanaoeneza siasa za uchochezi .
“Nataka kuwaomba leo
wachukieni wachochezi na pia niwaelezeni kuwa mimi si tajiri ila nina utajiri wa
watu na ushawishi na ninafanya mambo haya ili kumbukumbu yangu iweze kuandikwa
Mbinguni na nimekuwa nikialika watu wengi na nimekuwa nikifika wacha wenye
kusema waseme watasema ila usiku watalala wenyewe ….sitaacha kusaidia kwa
kuogopa kusemwa”
EmoticonEmoticon