WANAFUNZI WA SHULE YA WALEMAVU KATUMBA TWO WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA WANAHITAJI MSAADA WA KUJENGEWA CHOO CHA KISASA KINACHOENDANA NA ULEMAVU WAO KULIKO HIVI SASA WATOTO WANATESEKA NA KUJISAIDIA SEHEMU CHAFU NA SIO SALAMA KWA AFYA ZAO


HARI YA HEWA LEO MJINI TUKUYU

WANAFUNZI WA KATUMBA TWO SHULE MAALUM KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA VIUNGO, KUONA, KUSIKIA, ALBINO NA WALEMAVU WA AKILI



KWA UZALENDO WA WATU WA JAPANI KUPITIA UBAROZI WAO WAMEFADHIRI UJENZI WA MADARASA MAWILI NA MABWENI MAWILI KATIKA SHILE YA WALEMAVU KATUMBA

MABWENI MAWILI YA WATOTO WALEMAVU AMABAYO YANAJENGWA KWA HISANI YA WAJAPANI

SHIDA ILIYOPO HAPA NI UMBALI WA VYOO VILIPO NA MABWENI YA KULALA PIA MADARASA FIKILIA MVUA ZA TUKUYU NA MTOTO ANAYE TEMBEA KWA KUTAMBAA JINSI YA KUFIKA KUJISAIDIA NI SHIDA SANA

VYOO VILIVYOJENGWA NA SERIKALI NA KWAGHARAMA KUBWA VIMEISHIA KUBOMOKA HUKU WATOTO WAKITAABIKA KWA KUKOSA VYOO VINAVYOENDANA NA MAHITAJI YAO
HAWA WATOTO NDIO KWANZA WANAJISAIDIA KWA KUSIMAMA MLANGONI SASA INAPOTOKEA AMBAYE ANATEMBEA KWA KUTUMIA MIKONO NDIPO UTAONA HURUMA SANA MAANA CHOO KINAKUWA KICHAFU MAANA HAWA WALIO NA UWEZO WA KUSIMAMA WANAJISAIDIA HOVYO
CHOO NI KICHAFU NA MIUNDOMBINU SI RAFIKI KWA WATOTO WALEMAVU
WATOTO WANAHITAJI KUSAIDIWA NA WATANZANIA WALIO NA UZALENDO NA WATANZANIA HAWA WALIO NA MAHITAJI MAALUM U ILI WAFIKIE NDOTO ZA KUPATA ELIMU KAMA WENGINE
JAMANI MIUNDO MBINU YA HAPA SIO RAFIKI KWA WATOTO WETU
HIKI CHOO NI KIMEJENGWA TANGU MWAKA 2008 TANGU KIPINDI HICHO KIMEFIKIA HAPO
 NAKUMBUKA MWAKA 2008 NIKIWA NIMETOKEA CHUONI NIKAHAMASISHWA NA NDUGU YANGU MICHAEL MHAGAMA KUPITIA KAMPUNI YAKE YA UJENZI ILI TUSHIRIKI PAMOJA UJENZI WA CHOO JAPO ANGALAU KIWE RAFIKI KWA WATOTO WALIO NA ULEMAVU KATIKA SHULE HII YA KATUMBA TWO.

NAKUMBUKA KILA MFANYAKAZI  WA KAMPUNI ALIKUWA ANACHANGIA TSH 10,000/= NA KWA KIPINDI KILE TULIFANIKIWA KUJENGA CHOO CHENYE MATUNDU SITA NA MATANKI YAKE  PAMOJA NA MASINKI YAKE LAKINI BAADA YA UJENZI HUO MAMBO HAYAKUKAMILIKA ILI WATOTO WAANZE KUKUTUMIA CHOO.

KWAHIYO TANGU MWAKA HUO CHOO BADO HAKIJAKAMILIKA HASA MIUNDOMBINU YA MAJI NA KUPELEKEA CHOO HIKI KUTOTUMIKA. SASA IMENIBIDI NIFIKE TENA HAPA SHULENI KUJUA NINI KIMEBAKI ILI CHOO KIWETAYARI NA WATOTO WAENDELEE KUTUMIA KULIKO SASA WATOTO WETU HAWANA CHOO KINACHOENDANA NA ULEMAVU WAO

OMBI LANGU NI WADAU WA HUU MTANDAO KWA WALE WALIO NA MAPENZI MEMA KWA WATOTO WETU KUJITOKEZA ILI WATOTO WETU TUWAMALIZIE UJENZI WA CHOO PAMOJA NA MIUNDO MBINU YA KOLIDO LA KWENDEA CHOONI ILI KUJIKINGA NA MVUA, KULIKO WANAVYOTUMIA VYOO AMBAVYO VINASABABISHA WATOTO KUPATA MAGONJWA AU WANAPOISHIA KUJISAIDIA VICHAKANI

NIMEONGEA NA MKUU WA SHULE HII YA KATUMBA TWO ILI KUJUA GHARAMA ZA UJENZI ULIOBAKIA ILI KUJIPANGA KUMALIZIA CHOO HICHO AU KUJENGA KINGINE HIVYO AMENIAHIDI KUWA ATAMTAFUTA MTAALAM ILI TUJUE THAMANI YA VITU VILIVYOSALIA KUMALIZIA UJENZI WA CHOO HIKI.

MWL OMWILE KALYOTO MWALIMU MKUU WA SHULE MAALUMU YA WALEMAVU. MWALIMU KALYOTO AMESEMA KUWA WATOTO WALIOPO HAPO NI WALEMAVU WA VIUNGO, WALEMAVU WA KUSIKIA, WALEMAVU WA KUONA, WALEMAVU WA AKILI PIA NA WALEMAVU WA NGOZI YAANI ALBINO.
WATOTO WAKO MICHEZONI WAKATI WA MAPUMZIKO



MAZINGIRA DUNI YA KUJISOMEA KWA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUONA NA VIFAA DUNI HADI KUFIKIA KUTUMIA MAWE ILI KUJIFUNZA KUHESABU
KALAKANA YA KUTENGENEZEA VIATU VYA WATOTO WALIO NA ULEMAVU MBALIMBALI WA VIUNGO
WATOTO ZAIDI YA MIA MOJA AMBAO WANASHIDA YA KUONA WANAUHITAJI WA MASHINE HII YA KUANDIKIA LAKINI HAPO SHULENI PANA MASHINE TANO TU KITU KINACHOWAPA SHIDA SANA KUJIFUNZA. KWA WALIO NA MAPENZI MEMA HII MASHINE INAITWA BREILA NA DUKANI INAUZWA MILIONI MBILITU
PIA KUNA VIFAA MAALUM VYA KUHESABIA NA KALATTASI MAALUM ZA KUANDIKIA HAPA SHULENI NI SHIDA SANA KWA KUWA SHULE INAPATA BAJETI NDOGO SANA KUTOKA TAMISEMI AMBAYO HAIKIDHI MAHITAJI YA WATOTO SHULENI HAPO
SEHEM WANAPO LALA WATOTO
NIKAPATA NAFASI YA KUZUNGUMZA JAPAO NA WANAFUNZI WACHACHE KULICHONIFURAHISHA WATOTO HAWA NI KUTAMBUA KUWA SERIKALI INAWATHAMINI SANA KWA KUWA SERIKALI INAWAPA NAULI NA WALIMU WA KUWACHUKUA MAJUMBANI NA KUWARUDISHA SHULENI HAPO, PIA CHAKULA CHAO NI KIZURI NA ZAIDI WAKASHUKURU SANA WADAU WA SHULE HIYO WANAJITOKEZA KUWAHUDUMIA KWA MAVAZI , CHAKULA NA SASA WAFADHIRI WA KIJAPANI WANAOENDELEA NA UJENZI WA MADARASA MATATU NA UJENZI WA MABWENI MAWILI
SASA UKAFIKA WAKATI WA KILA MTU ANATOA MACHOZI MAANA WATOTO WALIO WENGI WAZAZI WAO NI KAMA WAMEWATELEKEZA KABISA HATA SALAMU WALA KUWATEMBELEA HIVYO WANAKABIRIANA NA MAISHA MAGUMU SANA KWA KUKOSA MAHITAJI YA MUHIMU KAMA MAVAZI, SABUNI, SALE ZA SHULE, VIATU NA HATA VIFAA VYA MADARASANI. HIVYO WAMEWATAKA WAZAZI WASIWATELEKEZE  KIASI HICHO KWAKUWA WAO WANA NDOTO ZA MAISHA KAMA WALIVYO WATOTO WATOTO WASIO NA ULEMAVU.
NAYE MWALIMU MKUU AMETHIBITISHA HILI KUWA WAZAZI WALIOWENGI HAWATAKI KUWAHUDUMIA WATOTO WAO WAKIWA SHULENI HIVYO WATOTO HUKOSA MAHITAJI YA MUHIMU HIVYO MAISHA YA SHULENI HAPO HUWA MAGUMU JAPO SERIKALI HUWAHUDUMIA WATOTO HAWA KWA KIASI KIKUBWA

WADAU NAKARIBISHA MAWAZO NIJINSI GANI TUPATE SURUHISHO LA WATOTO WETU ILI WAPATE CHOO CHA KISASA MAANA WAJAPANI WAMETUSAIDIA KUJENGA MADARASA MATATU NA MABWENI MAWILI NAMI NAJUA KWA HILI LA CHOO TUTALIWEZA. KARIBUNI KWA MICHANGO YA MAWAZO NA MALI PIA.
Previous
Next Post »