"TUNAJIANDAA KUGOMA KWA MARA NYINGINE TENA MPAKA KIELEWEKE"...CHAMA CHA WALIMU


Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimetaka Bunge na wazazi kuingilia kati uamuzi wa Serikali wa kukataa kukaa katika meza moja, kuzungumzia nyongeza za mishahara na posho.

Chama hicho kimesema, vinginevyo Serikali inakaribisha mgomo mwingine wa walimu.

Mwaka jana walimu nchini waligoma kufanya kazi wakishinikiza nyongeza za mishahara, lakini Serikali ilikimbilia mahakamani.

Kwa upande wake, mahakama ilisitisha mgomo huo kwa maelezo kuwa ulikuwa batili na baadaye, kuziagiza Serikali na CWT kukaa tena kwenye meza ya majadiliano.


Jana Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema pamoja na chama hicho kuwa tayari kuzungumza, Serikali imekataa kuzungumza nacho kuhusu nyongeza za mishahara na masilahi mengine ya walimu.

“Serikali imeeleza msimamo wake wa kutojadili masuala ya mishahara na posho kupitia majadiliano kwenye mabaraza ya kisekta, ikiwa ni pamoja na Baraza la Walimu,” alisema Mukoba akinukuu taarifa ya Serikali.

Alisema kwa taarifa hiyo Serikali imepuuza amri ya mahakama inayotaka pande hizo kukaa meza moja kwa sababu inafahamu kwamba haitachukuliwa hatua yoyote.


“Serikali haikujifunza chochote katika mgomo wa walimu uliopita na inatamani kuona mgomo mwingine mwaka huu, Bunge na wazazi tunaomba muingilie kati matatizo haya ya walimu,” alisema Mukoba.


Alisema walimu wakigoma watasababisha wanafunzi milioni 10 kukosa masomo
Previous
Next Post »