MFAHAMU RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA KIUNDANI AMBAPO LEO NI SIKU YAKE YA KUZALIWA


Jacob Gedleyihlekisa Zuma (* 12 Aprili 1942) ni Rais wa Afrika Kusini tangu 2009. Alikuwa makamu wa rais chini ya Thabo Mbeki kati ya 1999 na 2005. Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha ANC.
Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la KwaZulu-Natal. Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria). 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja na Nelson Mandela. Baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko Msumbiji na Zambia. Aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC.
Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990, Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha Natal na baada ya uchaguzi wa 1994 akawa waziri katika serikali ya jimbo.
Mwaka 1997 alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa ANC na mwaka 1999 akateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri.
Mwaka 2005 mshauri wake Shabir Shaik alihukumiwa miaka 15 jela kwa sababu alipokea rushwa. Zuma alishtakiwa pia na Rais Thabo Mbeki akamwachisha Umakamu wa Rais. Kesi hii ilisimamishwa kwa sababu mashitaka hayakuandaliwa vizuri. Kuna maandalizi ya kupeleka mashitaka mapya.
Miezi michache baadaye alishtakiwa tena kwa sababu mama mmoja alidai ya kuwa alinajisiwa na Zuma. Katika kesi hii Zuma hakuhukumiwa kwa sababu hakimu aliamini madai kwamba mama yule alikubaliana naye.
Mwaka 2007 Zuma akagombea nafasi ya mwenyekiti wa ANC dhidi ya Thabo Mbeki aliyetaka kuchaguliwa tena.
Zuma alishinda. Sasa anaaminiwa atakuwa pia mgomnbea wa urais upande wa ANC.
Previous
Next Post »