JACKLINE WOLPER AMUENZI KANUMBA KIPEE

 


MSANII wa filamu nchini Jacklne Wolper amuenzi marehemu Steven Kanumba kivingine kwa kutoa filamu ya 'After Death' ambayo ni mwendelezo wa filamu iliyochezwa na marehemu Steven Kanumba ikiwa ni moja ya kuviendeleza vipaji alivyoacha marehemu Kanumba
Filamu hiyo ambayo pia imezinduliwa siku ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja  tangu Kanumba afariki  April 7 katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya kuviendeleza vipaji vya watoto waliocheza na marehemu katika filamu ya Uncle JJ wanaojulikana kwa jina la Patrick na Jenifer
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Wolper alisema kuwa filamu hiyo aliiandaa katika mazingira maalumu kwa ajili ya kumuenzi Kanumba ambaye kila mtanzania anatambua mchango wake kukuza sanaa kiujumla
 
Alisema kuwa ameamua kumuenzi kwa kutoa filamu hiyo ya muendelezo wa filamu ya Uncle JJ na kucheza na watoto hao ili kuhakikisha anamuenzi kwa vitendo huku akimuombea alale mahali pema peponi

"Filamu ya Uncle JJ ni filamu ambayo yeye mwenye Kanumba alikuwa anaipenda na kuikubali sana hivyo kumuenzi kwa vitendo ni moja ya ya kukamilisha dhamira yake ambayo amejiwekea" alisema Wolper

Previous
Next Post »