WAZIRI MEMBE ATAJWA SALAKATA LA KUTESWA KWA MWENYEKITI JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

JINA la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaitafa, Bernard Membe, limeanza kuhusishwa na tukio la kutekwa na kuteswa kikatili na watu wasiojulikana lililomkuta Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda.
Madai ya kulihusisha jina la Waziri Membe na tukio hilo, yalianza kuzagaa miongoni mwa watu waliofika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Kibanda, muda mfupi baada ya kutendewa unyama huo.
Makundi ya watu waliokuwa hospitalini hapo walilioanisha tukio hilo na kauli iliyopata kutolewa na Waziri Membe katika mahojiano ya kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, alipoeleza kuwa anao maadui wakubwa 11, wakiwamo waandishi wa habari wawili ambao aliahidi kuwashughulikia.
Ingawa Membe alikutana na shinikizo la watu mbalimbali lililomtaka awataje maadui zake hao 11, wakiwamo waandishi wa habari wawili ambao alikuwa na mpango wa kuwashughulikia, hadi sasa hajapata kufanya hivyo, jambo ambalo linadaiwa na wadadisi wa mambo kuwa ni uamuzi wake wa kuchukua mkondo wa kutekeleza kile alichokisema kwa vitendo.
Previous
Next Post »