WATU 8,204 wenye virusi vya Ukimwi wamepotea mkoani Morogoro na kuacha kutumia dawa za kurefusha maisha ARVs kati ya watu 39,638 walioandikishwa katika kliniki na vituo mbalimbali vya afya kuanzia Oktoba 2004 hadi Desemba 2012.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Tunajali Tanzania linalohusika na masuala la mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU kwa ufadhili wa Shirika la USAID la nchini Marekani, umeonyesha kuwa katika kipindi hicho watu 24,881 walianza matumizi ya dawa, wakati 13,438 ndiyo walihudhuria kliniki hadi Desemba mwaka jana.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kitaalamu kutoka Tunajali makao makuu Dk Protas Ngayanga wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkakati wa kurejesha kwenye tiba watu wote wanaoishi na VVU ambao walisajiliwa kwenye vituo mbalimbali vya huduma na tiba hizo (CTCs) na baadaye kuacha kuzitumia.
Dk Ngayanga alisema kundi kubwa lililopotea ni lile ambalo lilipimwa na kuambiwa bado hawajafikia hatua ya kutumia dawa na hivyo kutakiwa kuhudhuria kliniki ili kuangalia maendeleo ya afya zao, ambao alidai imeonekana kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi kwa kuamini wako salama.
Aliyataja makundi mengine kuwa ni wale wanaotumia tiba mbadala, kuhama vituo, mambo ya kiimani ikiwamo matumizi ya dawa za asili.
“ Watu wengine wameacha kutumia dawa kutokana na imani zao wengine hata kukimbilia kikombe cha babu, jambo hili limewafanya kushindwa kurejea kwenye vituo na kuendelea na huduma,” alisema.
Kwa Upande wake Meneja wa Tunajali Mkoa wa Morogoro, DK Musa Ndile alisema jumla ya vituo 11 katika halmashauri mkoani hapa ambavyo vimeonekana kuwa na idadi kubwa ya waathirika vinatumika kama majaribio.
Meneja huyo alisema mkakati huo ni endelevu ambapo kamati za afya za mkoa na wilaya zitakuwa zikiendelea kufuatilia utoaji huduma hiyo, huku lengo likiwa ni pamoja na kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto huku wakiendelea kuboresha na kutoa vifaa katika vituo na maabara.

EmoticonEmoticon