MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
imesema inatarajia kuzima matangazo ya mfumo wa analojia mkoani hapa Februari
28, mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfumo
mpya wa utangazaji wa dijitali.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi
Gunze, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini
hapa.
Alisema matangazo rasmi ya mfumo wa dijitali mkoani hapa Machi mosi mwaka huu, na kwamba TCRA ipo kwenye mchakamchaka wa kutekeleza mipango yake ya makubaliano na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika suala zima la kujiunga na mfumo wa dijitali.
“TCRA tumepanga kuzima mitambo yote ya
analojia ifikapo Februari 28 mwaka huu saa 6 usiku kwa Mkoa wa
Mwanza.
Hata hivyo, aliwataka wananchi wa Mkoa wa
Mwanza kuondoa hofu kuhusu ving’amuzi vinavyouzwa na kusema kuwa yapo makampuni
matatu ambayo ni Star Media, Agape Association na Basic Transmission ambayo
yamepewa kazi ya kununua na kuuza vifaa hivyo nchini.
Kuhusu mikoa minne mipya ya Geita,
Njombe, Katavi na Simiyu, Gunze alisema mikoa hiyo itaanza kutumia mfumo wa
dijitali kuanzia mwakani, kwani kwa sasa serikali imeshatenga fedha kwa njia ya
ruzuku kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote kwa ajili ya ununuzi wa vifaa
vitakavyowezesha upatikanaji huo wa programu ya dijitali
EmoticonEmoticon