MAMA UWOYA: SASA NAMLEA KRISH KWA MAKUBALIANO MAALUM



 
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
MAMA mzazi wa Irene Uwoya, Naima Uwoya amefunguka kuwa sasa anamlea mjukuu wake Dagraei Krish kwa makubaliano maalum.
Akizunguma na Ijumaa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar, mama huyo alisema maneno yanayoenezwa mitaani kwamba wao (wazazi wa Uwoya) wamempiga ‘stop’ Irene kumchukua mtoto kufuatia mabadiliko ya tabia zake si ya kweli na kwamba wanachokifanya ni kutimiza majukumu yao kama wazazi.
“Irene ni mtu mzima na ana akili zake ndiyo maana akazaa, sisi hatuna tatizo naye na nashangaa maneno mengi yanayosemwa na watu yanatoka wapi. Wanaosema hivyo ni rafiki zake ambao ni wanafiki tu lakini sisi tunamlea mjukuu wetu kwa makubaliano maalum na kwa mapenzi yetu,” alisema mama Uwoya.
Awali, kulikuwepo na madai kuwa Uwoya amezuiwa kumchukua mwanaye na kutotumia magari ya familia eti kutokana na ‘umcharuko’ wake baada ya kuwa mbali na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’
Previous
Next Post »