Dola 377,000 zatumika kununua iPad bungeni


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
BUNGE nchini Uganda limetumia zaidi ya dola 377,000 kununa kompyuta aina ya iPad kwa ajili ya wabunge wote .
Maofisa wa bunge hilo walisema kuwa mbali na kuwaweka wabunge hao karibu na ulimwengu wa teknolojia, wanatarajia kuwasaidia kupunguza gharama za fedha zinazotokana na matumizi ya uchapishaji wa nyaraka mbalimbali.
Kamishna wa bunge hilo Elijah Okupa alisema kuwa kompyuta hizo ni bora na zinafaa kwa matumizi hivyo ni vyema zikatumiwa vizuri.
Alisema iPad hizo zitakuwa ni mali ya wabunge lakini kama mtu atatumia kwa muda wa miaka mitano asitegemee itakuwa na ubora uleule wa kumwezesha mwingine atumie kwa miaka hiyo alisema Okupa
Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika bunge hilo zilionyesha Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya dola 12 katika miaka miwili sasa kwa ajili ya mahitaji ya kama kompyuta, uchapishaji wa nyaraka, mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kuwa bora katika bunge.
Kwa mujibu wa mbunge kutoka mashariki, Medard Segona alisema kuwa kutokana na uwepo wa ipad hizo wanategemea kupunguza matumizi ya fedha zilizokuwa zikipotea hapo awali.
‘’Vifaa hivyo vitapunguza sana matumizi ya fedha kwa kuwa hapo awali wizara ya fedhailikuwa ikichapisha zaidi ya nyaraka 400 kwa kila mbunge na maofisa wengine waliopo ndani ya bunge hilo’’alisema
Aliongeza kuwa komputa hizo ni muhimu kwa utendaji kazi hasa katika kipindi hicho cha kuendeleza matumizi ya teknolojia.
Hata hivyo taarifa zilisema kuwa wabunge hao bado hawana uelewa mzuri juu ya matumizi hayo licha ya kuwa kampuni imeahidi kutoa mkataba wa mafunzo ambayo pia yatasaidia kupunguza gharama za matumizi.

Previous
Next Post »