NASEMA KWAMBA "BILA MILIONI 10 HACHEZI FILAMU YA MTU"- ROSE NDAUKA


Msanii Rose Ndauka ni mmoja kati nyota wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu bongo, ambapo amedai kuwa baada ya kushiriki kwenye filamu nyingi na kuonesha uwezo wake sasa kama kuna mtu anayehitaji kumtumia ndani ya kazi yake basi lazima awe na shilingi milioni 10 cash mbali na hapa itakuwa ngumu kushiriki.

Kiwango cha fedha cha msanii huyo inaonyesha kuwa anajua thamani yake kama msanii mkubwa anayehitaji kuwa lulu ndani ya tasnia hiyo. Baadhi ya filamu alizowahi kung’arisha mwanadada huyu ni pamoja na ‘Because of You’‘Love Me Or Love Me Not’ na nyingine nyingi.

Rose alifunguka na kudai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuficha na kuendelea kuumia, na ndiyo maana ameamua kuweka wazi ishu hiyo kuwa hachezi filamu ya mtu bila muafaka wa kiwango cha fedha alichokitaja.

“Inatakiwa tufikie kipindi wasanii tujue thamani yetu kwani wapo baadhi ya wasanii wengine wana majina makubwa lakini wanafanya filamu kwa bei za chini, lakini siwezi kulaumu kwani kila mtu anafanya kwa mipango yake,” 
 
Previous
Next Post »