Watu
wawili wamefariki dunia Mkoani Mbeya katika matukio mawili likiwemo la
mwanafunzi kunywa sumu inayosadikika kuwa ni sumu ya panya,baada ya
kufokewa na Bibi yake kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.
Tukio
hilo limetokea Agosti 18 mwaka huu majira ya saa mbili usiku Shukrani
Ndembo(18) mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari
Isange na Mkazi wa Kitongoji cha Ndamba,Kijiji cha Isange,Wilayani
Rungwe amejikuta akipoteza uhai wake baada ya kunya sumu hiyo.
Sakata
hilo lilianzia pale Bibi wa marehemu alipomtuma binti huyo dukani
kununua mahitaji na kisha kuchelewa kurudi nyumbani na baada ya kuulizwa
marehemu aliamua kuchukua sumu na kuinywa,ambapo hali yake ilikuwa
mbaya na juhudi za kumkimbiza hospitalini zilifanyika lakini ziligonga
ukuta baada ya marehemu kufikwa na mauti muda mfupi.
Mwenyekiti
wa Kijiji hicho Bwana Lutengano Mwakyoma, amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kisha kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha wilaya
hiyo,ambapo walifika na kuthibitisha tukio hilo.
Hilo
ni tukio la pili kutokea kwa wanafunzi wa shule mwaka huu,ambapo
mwanzoni mwa mwaka mwanafunzi mwingine alifariki dunia baada ya kugundua
kuwa ana ujauzito.
Aidha,mnamo
majira ya saa 10 jioni Agosti 20 mwaka huu,katika Kijiji cha
Ihanda,Wilayani Mbozi barabara ya Mbeya/Tunduma gari nambari T 466 BGF
aina ya Toyota Coaster linalosafirisha abiria kutoka Mbeya mpaka Tunduma
lilimgonga mtembea kwa miguu Moto Asha Mzumbwe(8) na kusababisha kifo
papo hapo.
Hata
hivyo chanzo cha ajali ya gari hilo lililokuwa likiendeshwa na dereva
Bwana Michael Kasebele(56),mkazi wa Kalobe Jijini Mbeya,kimetajwa kuwa
ni kuwa ni mwendokasi wa kupindukia.
Kamanda
wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athuman amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na ametoa wito kwa wazazi kuchukua tahadhari ya kutowaacha watoto
wao kurandaranda barabarani.
Tukio
hilo nila kwanza tokea kuwekwa kwa matuta katika eneo la Ihanda,baada
ya magari mengi kusababisha vifo vya mara kwa mara kwa wananchi wa eneo
hilo,ambapo walifikia hatua ya kulichoma moto gari ya abiria aina ya
Coaster kutokana na mwendokasi.
EmoticonEmoticon