Mabaki ya helikopta ya Uganda yapatikana Kenya
Juhudi za
kuwatatuta wanajeshi saba wa Uganda wanaodhaniwa wamenusurika na ajali
ya helikopta ziliendelea Jumanne huko mlima Kenya
Simon Gitau, naibu mkuu katika idara ya mbuga ya kitaifa ya Mt. Kenya amesema timu ya waokozi ilipata maiti mbili nje ya helikopta hiyo ambayo ilikuwa bado inaungua moto Jumanne na kwamba kuna uwezekano wa kupata maiti nyingine ndani ya helikopta hiyo.
Msemaji wa wizara ya Ulinzi nchini Kenya Bogita Ongeri, anasema wameshapata helikopta zote tatu zilizoanguka wamezipata, na juhudi zinaendelea kuwatafuta wanajeshi watano ambao hawajajulikana walipo.
EmoticonEmoticon