PISTORIUS KUPIMWA AKILI


AP_Pistorius_1404047_DG_16x9_992
Jaji mmoja wa Afrika Kusini ametoa amri kwa mwanariadha Oscar Pistorius kufanyiwa vipimo vya akili na kusimamisha kesi inayomkabili ya mashitaka ya kumuuwa rafiki yake wa kike mwaka jana nyumbani kwake.
Jaji Thokozile Masipa alitopa maamuzi yake jumatano , kufuatia ushahidi uliotolewa wiki hii kutoka kwa shahidi mmoja wa upande wa utetezi aliyesema kwamba Pistorius alikuwa na ugonjwa wa kuchanganyikiwa ambao unasababisha wasi wasi na woga.
Mwendesha mashitaka Garry Nel aliomba vipimo hivyo .Anasema hataki Pistorius kutumia hali hiyo kuwa ni uwezekano wa kukata rufaa huko mbeleni.
Jaji huyo amesema Jumatano vipimo hivyo ni vya kuhakikisha kwamba Pistorius anapewa haki yake kwenye kesi hiyo na kwamba ataangaliwa bila kulazwa . Atatoa taarifa kamili juu ya amri hiyo kesi hiyo itakaposikilizwa tena .
http://www.voaswahili.com
Previous
Next Post »