
Serikali ya Misr imetangaza amri ya
dharura kote nchini kuanzia hii leo, kwa muda wa mwezi moja kufuatana na
taarifa ya rais iliyotangaza na televisheni ya taifa.
Taarifa hiyo ina liamrisha pia jeshi kukisaidia kikosi cha polisi "kutanzua mzozo unaotokea kote Misri."
Taarifa hiyo imetolewa wakati vikosi
vya usalama vilikuwa vinashambulia makambi mawili kuwaondowa wafuasi wa
rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi kati kati ya mji mkuu wa
Cairo.
Wakati huo huo kumekuwepo na ripoti
zinazotofautiana hii leo juu ya idadi ya watu walouliwa na walojeruhiwa
katika ghasia zinazotokea kote nchini. Wizara ya afya inaeleza watu 95
wameuliwa na wengine 974 kujeruhiwa kote nchini.
hata hivyo baadhi ya wanachama wa
chama cha Muslim Brotherhood cha Bw Morsi wanasema idadi ya walofariki
imefikia hadi 2,200 na wengine elfu 10 kujeruhiwa. sauti ya amerika
haijaweza kuthibitisha idadi hizo zote zinazotolewa.
EmoticonEmoticon