''Afande Mapembe'' (Baba Kundambanda)
Kwa
wadau wa vichekesho hapa nchini nadhani walio wengi wanamfahamu msanii
huyu kutokana na umaahiri wake wa uchekeshaji kwa swaga za kimakonde,
Wengi mnamtambua kwa jina ''Mapembe'' almaarufu ''Baba kundambanda'', Hususani wale mnaofatilia kipindi cha ''VITUKO SHOW'' kinachorushwa na runinga ya ''CHANNEL TEN'' Kila siku ya alhamisi saa mbili na
nusu usiku au wale mnaofatilia filamu za vichekesho zinazoandaliwa na kampuni ya Al-Riyamy Production
chini ya mkurugenzi wa kampuni hio ''Alphan ''Nassoro Abdala''. Baba
kundambanda yuko hoi bin taaban kupitia ugonjwa ambao haujatambulika
mpaka sasa! akiwa kambini Jijini Tanga huko wasanii wa kundi hilo
walikoweka kambi ya takribani miaka miwili sasa,. Wasanii hao wa kundi
la ''VITUKO SHOW''
wakiwa katika maandalizi ya kipindi na filamu za vichekesho, ndipo
mwenzao alipoanza kuumwa gafla na kuzidiwa! mpaka sasa hali yake ni
utata ila anaendelea kufatilia vipimo mwenyezi mungu atamjalia atapona
na kuendelea na kazi kama kawaida upone haraka
Baba kundambanda.
Source:Masai Nyotambofu
EmoticonEmoticon