JOSE MOURINHO: NAIPENDA LONDON …Akaa mkao wa kula kurejea Chelsea

JOSE MOURINHO: NAIPENDA LONDON …Akaa mkao wa kula kurejea Chelsea

KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amefichua kuwa anaipenda London na kwamba huenda siku moja akarejea Chelsea.
Mourinho kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011, juzi usiku alikuwepo kwenye uwanja wa Stamford Bridge kushuhudia mechi ya kirafiki ya Brazil na Urusi.
Kocha huyo mwenye makeke alithibitisha kuwa siku moja angependa kurejea England - hususan kazi yake ya zamani.
Mourinho alisema: “Ninakuja London mara nyingi kwa sababu tuna nyumba hapa, tunapapenda na binti yetu anakuja kusoma London.
“Hisia zangu zinaguswa na Chelsea kwa kiasi kikubwa na siku moja nitajikuta nimerejea kwenye soka la Uingereza aidha kwa Chelsea au klabu nyingine yoyote.
“Sio siri Chelsea ina maana kubwa kwangu kuliko timu zingine, Chelsea ipo ndani ya moyo wangu kama ilivyo kwa Inter Milan. Siku moja lazima nirejee.
Hata hivyo Mourinho alisisitiza kuwa anandelea kuwa mtiifu kwa kibarua chake cha Real Madrid – angalau mpaka mwisho wa msimu.
Previous
Next Post »